Posts

Showing posts from July, 2018

RUSIA FIFA 2018

Image
Neymar jr yupo kwenye wakati mgumu sana katika mchezo wa mpira kufuatia timu yake ya taifa ya Brazili kutolewa na Ubelgiji katika hatua ya robo fainali kwenye mashindano yanayoendelea huku Urusi katika msimu wa mwaka 2018.Staa huyo anaekipiga ligi ya Ufaransa katika klabu ya Paris saint german almaarufu (PSG) licha ya kuwa na wakati mgumu katika timu yake ya taifa lakini pia anafikilia zaidi huenda hali hii ikamsumbua hadi kwenye klabu take anayochezea."Tulipambana kwa kila hali ili kuhakikisha tunafika mbali zaidi na kufikia hatua ya fainali na kupata heshima kubwa kutwaa kombe la dunia kwa msimu huu,lakini imekuwa tofauti na tulivyo tarajia hatukati tamaa ni wakati wetu sasa kujipanga kwa mashindano yajayo.Napata wakati mgumu sana lakini naamini MUNGU ataniongoza na kusahau yaliyotokea".alisema Neymar katika mahojiano na waandishi wa habari nchini Urusi mda mchache kabla ya kuondoka kwa timu yake kurudi Braziri.