SOCCER
Morinho:sina ugomvi na pogba.....
Kocha mkuu wa kablu tajiri iliyo na makazi yake jijini Uingereza mashetani wekundu,MANCHESTER UNITED the special one Jose Morinho amekanusha uvumi ulioenea zaidi kwenye mitandao kuwa yeye na kiungo wa kati wa klabu hiyo Pogba kwamba wako kwenye mgogoro na mawasiliano yasiyo mazuri.Morinho alikili kuwa Pogba hakuganya vizuri katika mechi iliyo wakutanisha Manchester united na Newcastle united ambapo katika mechi hiyo Morinho alikubali kipigo cha goli kwa bila.Lakini pamoja na kocha huyo kujitetea kuwa hawana ugomvi tetesi zimesambaa kuwa Pogba kwa sasa hachezeshwi katika nafasi yake bali huchezeshwa katika safu isiyo na mashambulizi ndio maana anashindwa kufanya vizuri zaidi.
Morinho aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa"sio kweli kwamba mimi na mchezaji wangu Pogba tuna ugomvi na sio kweli kwamba mimi na yeye hatuna mawasiliano mazuri,ningependa kusema kuwa huo ni uvumi tu na hauna ukweli wowote ninachojatibu kufanya ni kuimarisha kiwango cha Pogba nakumfanya awe bora zaidi".
MANCHESTER UNITED wanashuka dimbani leo kuchuana na UNDERFIELD katika kuwania kombe la FA katika uwanja wao wa nyumbani OLD TRAFFORD baada ya mechi yao ya kwanza iliyo chezwa katika uwanja wa nyumbani wa UNDERFIELD huku wenyeji hao wakikubali chapo cha goli nne kwa bila kutoka kwa mashetani wekundu.
Comments
Post a Comment