SOCCER

Manchester united klabu ya jijini Uingeleza ikiwa nyumbani katika uwanja wao wa Old Trafold wamewachapa wapinzani wao klabu ya Leicester city magoli mawali kwa moja.Mchezo huo ulionekana kumilikiwa na pande zote mbili kwa kipindi cha kwanza lakini klabu ya Manchester waliongeza kasi zaidi ya ushambuliaji huku wakifanikiwa kupata goli la kuongoza kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na kiungo maalufu na pia ni nahodha wa klabu hiyo Poul Pogba.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika klabu ya Manchester  United walikuwa mbele kwa holi moja,kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi huku Leicester city wakitafuta goli la kukomboa kwa nguvu zaidi na upande wa Manchester United wakilazimisha kuongeza magoli mengi.Hatimae klabu ya Manchester United wanafanya shambulizi kali la kishitukiza huku Alex Sanchez akitoa pasi kwa Juan Mata na kisababisha klosi kwa Shaw ambae anafanikiwa kiuweka mpira nyavuni.Leicester city wanafanya mashambulizi yasiyozaa matunda lakini katika dakika za nyongeza Vard anaipatia klabu yake goli la kwanza na kupata nguvu ya kurudisha mengine.Hadi dakika za nyongeza kumalizika klabu ya Manchester United wanaibuka na ushindi wa magoli mawaili huku klabu ya Leicester city wakiwa na goli moja.Kwa mujibu wa matokeo ya leo Manchester United wanaongoza ligi jijini Uingeleza .


Comments

Popular posts from this blog

LOWASSA AACHIWA HURU

MAN U VS LIVERPOOL