TOTTENHAM HOTSPUR VS NEWCASTLE UNITED

Lei katika ligi kuu ya Uingeleza mechi kadhaa zilipigwa na moja kati ya mchezo ulivuta hisia za wengi ni kati ya klabu ya Tottenham Hotspur dhidi ya wenyeji Newcastle United.Klabu zote zilionekana kuingia kwa kasi zaidi kuhakikisha kila mmoja anapata matokeo mazuri ndani ya dakika za mwanzo,hadi dakika ya nane Tottenham wanafanya shambulizi la kushitukiza lakini mlinda mlango wa klabu ya Newcastle anaokoa na kuipa kona Tottenham.Vertonghen anafanikiwa kuuzamisha mpira ndani ya nyavu za Newcastle nakuipatia klabu yake goli la kuongoza,wachezaji wa Newcastle wanapata nguvu wanafanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Tottenham moja kati ya shambulizi lao linazaa matunda.Ndani ya dakika ya kumi na moja kipindi cha kwanza Joselu anaunganisha kwa kichwa klosi iliyopigwa na mshambuliaji mwenzie,Joselu anaipatia klabu yake goli la kusawazisha.
 Mchezo ulionekana kuwa sawa katika pande zote mbili lakini vijana wa Tottenham Hotspur wanafanya shambulizi lingne na kufanikiwa kupata goli la pili la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao D.Alli ndani ya dakika ya kumi na nane kipindi cha kwanza.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Tottenham Hotspur wanaongoza goli mbili dhidi ya wenyeji Newcastle United ambao walikuwa na goli moja.Kipindi cha pili konaanza na mashambulizi yanaelekezwa langoni mwa timu zote kuonesha kwamba Newcastle wanataka kukomboa goli lakini huku vijana wa Tottenham Hotspur wakitaka kuongeza magoli mengi zaidi.Hadi dakika tisini zinamalizika matokeo ya abaki vile vile Tottenham Hotspur goli mbili na huku Newcastle United goli moja.Kwa mujibu wa matokeo ya leo Manchester United inaongoza ligi kwa kuwa na alamatatu ikifuatiwa na Tottenham Hotspur wakiwa na alama tatu pia kwa tofauti ya silabi.

Comments

Popular posts from this blog

LOWASSA AACHIWA HURU

MAN U VS LIVERPOOL