TOTTENHAM HOTSPUR VS NEWCASTLE UNITED
Lei katika ligi kuu ya Uingeleza mechi kadhaa zilipigwa na moja kati ya mchezo ulivuta hisia za wengi ni kati ya klabu ya Tottenham Hotspur dhidi ya wenyeji Newcastle United.Klabu zote zilionekana kuingia kwa kasi zaidi kuhakikisha kila mmoja anapata matokeo mazuri ndani ya dakika za mwanzo,hadi dakika ya nane Tottenham wanafanya shambulizi la kushitukiza lakini mlinda mlango wa klabu ya Newcastle anaokoa na kuipa kona Tottenham.Vertonghen anafanikiwa kuuzamisha mpira ndani ya nyavu za Newcastle nakuipatia klabu yake goli la kuongoza,wachezaji wa Newcastle wanapata nguvu wanafanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Tottenham moja kati ya shambulizi lao linazaa matunda.Ndani ya dakika ya kumi na moja kipindi cha kwanza Joselu anaunganisha kwa kichwa klosi iliyopigwa na mshambuliaji mwenzie,Joselu anaipatia klabu yake goli la kusawazisha. Mchezo ulionekana kuwa sawa katika pande zote mbili lakini vijana wa Tottenham Hotspur wanafanya shambulizi lingne na kufanikiwa kupata goli la pi...