SOCCER
Messi afungiwa mechi nne za kimataifa.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi amefungiwa mechi nne za kimataifa baada ya kumtukana mwamuzi msaidizi katika mchezo uliopigwa mjini Buenos Aires kati ya timu ya Argentina na Chile iliyochezwa alhamisi.
Shirika la mpira la dunia FIFA limetangaza hukumu hiyo saa chache kabla ya mechi kati ya Argentina na Bolivia kufuzu kombe la dunia mwaka ujao.Baada ya kumkosa Messi Argentina walifungwa goli mbili na timu ya Bolivia,magori ya Bolivia yalifungwa na wachezaji Juan Carlos na Marcelo Martins mchezo uliopigwa katika mji wa La Paz.
Comments
Post a Comment