MAPENZI

Mapenzi ni safari tamu sana ya upendo mambayo kamwe haiwezi kukosa huzuni furaha,majonzi na faraja.Maana halisi ya mapenzi ni jinsi unavyomjali mtu zaidi ya unavyoijali nafsi yako,mapenzi ni furaha amani na upendo.Wapo wanaoamini et hakuna mapenzi ya kweli hakika wao wanakosea mapenzi ya kweli yapo.Wengi wetu tunaingia kwenye mahusiano ya Kumapenzi bila kujua lengo halisi la kuingia huko ndio maaana wengi tunaishia kuumia,kulia,majuto na kupotezewa muda.Unapoamua kuingia kwenye mahusiano inamaana unaandaa maisha maisha yako ya badae na huyo mapenzi wako na upo tayari kukabiliana na kila changamoto itakayojitokeza hadi pale lengo lenu litakapotimia.Soma hizi kanuni 10 naamini utajifunza kitu.
(1)Kuamini kuwa upendo wakweli upo:unatakiwa kujiamisha kuwa unapendwa ha hakuna mwingine zaid yako,itakusaidia kupunguza fikra potofu za usaliti na itajenga uaminifu zaidi.
(2)Mawasiliano:kuwasiliana na mpenzi mara kwa mara hujenga ukaribu kati yenu hatakama mpo mbali,kujuliana hali humuaminisha mtu kuwa yupo kwenye fikra zako na umemuhifadhi moyoni hatakama upo mbali nae.
(3)Kutatua matatizo:matatizo ni sehemu ya mapenzi, kila litokeapo tatizo jaribuni kukaa kwa pamoja kujua chanzo cha tatizo kisha kutafuta njia za kulitatua.kamwe usichukue maamuzi ya kumuacha mpenzi wako kwasababu ya mapungufu yake kwani hakuna binadamu mkamilifu.
(4)Kumpa Uhuru:binadamu anasifa ya kufanya kitu ambacho moyo na akili yake vimeridhia,hyo ni kweli usimbane,usimfuatilie sana,usimpime sana kama anakupenda wala usimchunguzechunguze sana.Hii itaepusha ugomvi wa mara kwa mara na kukufanya uishi kwa amani bila mawazo.
(5)Kumshauri:ni kweli kwamba hakuna aliyekamilika unapoona mapungufu ya mpenzi wako usisite kumueleza kisha kumshauri chakufanya ili ajirekebishe.Hii itakusaidia sana kuwa jasiri na imara malinzi wa penzi lenu ni wewe wala simwingne.
(6)Maneno matamu:maskio ya mwanadamu yanapenda sana kuskia mambo mazuri na matamu.Unapokuwa na mpenzi wako karbu au hatakama yupo mbali jaribu kuongea nae kwa kumpa maneno matamu.Hakika hii itamfanya ajihisi wapekee na anayependwa zaidi,itamfanya asijute kuwa nawe.
(7)Kumjari na kumthamini:mfanye mpenzi wako kuwa mtu wathamani kwamba hakuna kitu muhimu kinachokupa furaha kama yeye,kwamba kati ya vitu usivyopenda kuvipoteza yeye ni wakwanza.hii itamfanya awekarbu sana na wewe ataamini kuwa hakuna upendo mwingine ila ni kwako tuu.
(8)Kujadili maisha ya badae:unapokuwa na mpenzi wako au unapiwasiliana nae jaribuni kujiri zaidi jinsi maisha yetu yatakavyokuwa hapo badae,kumuuliza anapenda kuishi mkoa gani,anapenda maisha yenu yaweje,anapenda muwe na watoto wangapi.Hii itamfanya asikuchoke na itamuongezea hamu yakuwa na wewe karibu hadi malengo yatimie.
(9)Kupigania unachokiamini:Hakuna kitu bora katika maisha kama akupigania unachokiamini,kama umempenda kweli mpenzi wako kwa dhati haijalishi mtapitia mambo mangapi ya kukatisha tamaa.Mpiganie kwa kila hali kuhakikisha unakuwa nae hadi mwisho usikubali kumpoteza mpenzi wako kirahisi.
(10)Angalia watu wa kuwashirikisha katika mahusiano yako:sio kila mtu anapenda  kukuona unadumu na mpenzi wako,hata ndugu yako wa tumbo moja pia anatosha kulitenganisha penzi lenu.Kuwa makini unapomshilikisha mtu unaemwamini.ila kumbuka usimwamini mtu yeyeto kwani huwezi jua moyo wa mtu unania gani.
HAKUNA KITU BORA KAMA KUINGIA KWNYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI MAPEMA ZAIDI KABLA YA NDOA.UNAPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO MAPEMA ILI KUTENGENEZA NDOA ILIYO IMARA ZAIDI.KITU MUHIMU NI KUISHI NA MPENZI AMBAE UME SHEA NAE FURAHA,HUZUNI KWA PAMOJA.HAKIKA HAPO UTAKUWA UMETENGENEZA MAHUSIANO YALIYO THABITI.....
TUTAKUJA KUONA KWANINI KUCHATI NA MPENZI WAKO KUNAONGEZA RADHA YA PENZI KULIKO KUONGEA NAE KWA SIMU..

Comments

Popular posts from this blog

LOWASSA AACHIWA HURU

MAN U VS LIVERPOOL